Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, marehemu Allama Misbah katika moja ya hotuba zake alijibu shubha iliyohusiana na “heshima ya kimungu kwa wanadamu dhalimu”, ambayo tunaiwasilisha kwenu kama ifuatavyo.
Swali: Je, Uislamu unawatambua viongozi wa Israel, wanaoua watu wasio na hatia kwa namna hii, kuwa na heshima ya kibinadamu? Au hawa ni wabaya zaidi kuliko mbwa mwitu wakali?
Jibu: Naam, Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu heshima – heshima ambayo Yeye Mwenyewe amemtunuku mwanadamu; lakini wakati mwingine mwanadamu huiondoa heshima hiyo kwa mikono yake mwenyewe.
Mwanadamu ambaye kwa mikono yake anatenda jinai mbaya zaidi, hufuta heshima aliyopewa na Mwenyezi Mungu.
Kwa sababu hiyo, yule yule Mungu aliyempatia mwanadamu heshima, wakati mwingine huamrisha auawe, na wakati mwingine pia huamrisha achomwe moto tuna mifano ya hali kama hizi.
Kwa hiyo, si sahihi kutuambia moja kwa moja kwamba heshima ni thamani isiyo na mipaka na kwamba kila mwanadamu ana heshima. Mwenyezi Mungu mwanzoni amewapa wanadamu wote heshima, lakini baadhi ya wanadamu huiondoa wenyewe heshima yao.
Chanzo: Marehemu Ayatollah Misbah Yazdi, 27/07/1388 (kwa kalenda ya Hijria Shamsia)
Maoni yako